Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars ) Mart
Nooj, ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini kujiandaa na
mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika uwanja wa CCM
Kirumba jijin Mwanza Machi 29, 2015.
Taifa Stars inayotarajia kucheza na The Flames mwishoni mwa
mwezi huu, itaingia kambini machi 22 machi
katika hotel ya Tansoma kujiandaa na mchezo huo kabla ya kuelekea jijini
Mwanza machi 24 kwa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo.
Wachezaji walioitwa kuingia kambini kujiandaa na mchezo huo
ni; Magolikipa, Deogratius Munish
(Yanga), Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Shomari Kapombe,
Erasto Nyoni, Aggrey Morris (Azam FC), Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa
Sugar), Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na
Hassan Isihaka (Simba SC).
Viungo ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha
Khamis (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo
(Stand United), washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry - Qatar),
Saimon Msuva , Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu,
Mbwana Samatta (Tp Mazembe - Congo DR), John Bocco (Azam FC), na Juma Luizio
(Zesco United - Zambia)
Timu ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza
machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka
la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.
Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA
Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na
kushika nafasi ya 100.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni