Mkataba wa Ayew katika klabu hiyo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na winga huyo ameweka wazi kuwa anataka kuondoka katika timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Ayew mwenye umri wa miaka 25 aligoma kuweka saini ya mkataba mpya jambo ambalo lilizivuta klabu kadhaa kubwa barani Ulaya zikiwemo Manchester United, Arsenal na Liverpool.
Akihojiwa Labrune amesema pamoja na umuhimu wa Ayew katika kikosi chao lakini hawataweza kumbakisha kwasababu hawawezi kummpa ya fedha kama za vilabu vya Ligi Kuu.
Labrune aliendelea kudai mfumo wa kifedha nchini Ufaransa in tofauti hivyo hawawezi kumpa fedha kama ambazo ataweza kuzipata akienda Uingereza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni