Messi akishangilia goli la ubingwa
LIONEL
Messi amewapa Barcelona ubingwa wa La Liga msimu wa 2014/2015 baada ya
kuifungia bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Atletico
Madrid kwenye uwanja wa Vicent Calderon.
Messi amefunga goli hilo katika dakika ya 65' akimalizia pasi ya Pedro Rodriguez.
Kwa matokeo hayo Barcelona wamefikisha pointi 93 baada ya kushuka dimbani mara 37 na wamebakiza mechi moja.
Real Madrid wameshinda magoli 4-1 dhidi ya Espanyol na kufikisha pointi 89 katika mechi 37 walizocheza.
Kwa maana hiyo wakishinda mechi ya mwisho watafikisha pointi 92 ambazo tayari zimeshavukwa na Barcelona .
Inawezekana
msimu ukawa mkubwa kwa Barcelona, leo wameshatwaa taji la ligi kuu, La
Liga na watacheza fainali mbili, ligi ya mabingwa ulaya na kombe la
mfalme 'Copa del Rey'.
Licha
ya kuugulia maumivu ya kutolewa nusu fainali ya Uefa na Juvuntes
katikati ya wiki hii na leo kukosa ubingwa wa La Liga, mshambuliaji
hatari wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga magoli matatu peke
yake 'hat-trick' katika ushindi wa Madrid.
Ronaldo
amefunga magoli hayo katika dakika ya 59', 83' na 90'. Goli lingine
limefungwa na Marcelo dakika ya 79' wakati goli la kufutia machozi kwa
Espanyol limefungwa na Cristian Stuani dakika ya 73''.
MATOKEO YOTE YA LA LIGA JANA USIKU HAYA HAPA:
FT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni