Herrera akifunga goli lake
MANCHESTER
United ikiwa uwanja wa nyumbani wa Old Trafford imetoka sare ya 1-1
dhidi ya Arsenal katika mechi ya ligi kuu England iliyomalizika usiku
huu.
Ander Herrera katika dakika ya 30' alipata pasi nzuri kutoka kwa Ashley Young na kuifungia Manchester United bao la kuongoza.
United
wakiwa na matumaini ya ushindi, dakika ya 82' Tayler Blackett
aliyetokea benchi alijifunga goli katika harakati za kuokoa na kufanya
mechi hiyo imalizike kwa sare hiyo.
Kama ilivyo kawaida kwa mechi za karibuni, United waliongoza umiliki wa mpira kwa 58% dhidi ya 42% za Arsenal.
Mbali
na hilo, United wamepiga mashuti 6 dhidi ya 4 yaliyolenga lango, wakati
ambayo hayakulenga lango, mashetani wekundu wamepiga 6 dhidi ya 2 ya
Gunners.
Hata hivyo kila timu imepiga kona 5 katika mechi hiyo iliyovuta hisia za mashabiki wengi.
Matokeo
haya yanaonesha wazi kuwa Man United watamaliza nne bora, wakati
Arsenal watamaliza nafasi ya pili na Man City nafasi ya tatu.
HUU NDIO MSIMAMO
JISOMEE MWENYEWE TAKWIMU ZA MECHI HIYO....
statistics :
6
shots on target
4
6
shots off target
2
58
possession (%)
42
5
corners
5
8
offsides
2
16
fouls
8
1
yellow cards
0
7
goal kicks
2
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni