Kocha
wa Chelsea Jose Mourinho amechaguliwa kuwa kocha bora wa msimu ligi
kuuu nchini Uingereza akiungana na mchezaji wake Eden Hazard ambaye
alichukua tuzo ya mchezaji bora wa msimu.
Mourinho
ameisaidia Chelsea kutwaa taji la kwanza la ligi kuu nchini Uingereza
baada ya kulikosa kwa takribani miaka mitano huku wakivunja rekodi ya
kukaa kileleni kwa kukaa siku 274.
Hii
ni mara ya tatu kwa Mreno huyo kutwaa taji hilo pamoja na kutajwa kama
kocha bora wa msimu. Aliwahi pia kutwaa mwaka 2004-05 and 2005-06.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akisherehekea kushinda tuzo ya kocha bora wa ligi kuu nchini Uingereza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni