Mpira
wa bara la Ulaya utakuwa na mabadiliko makubwa sana kama ikitokea
Lionel Messi anaondoka Barcelona, hii ni kauliya kocha wa Chelsea Jose
Mourinho.
Messi
amekuwa ni mtu muhimu sana katika klabu ya Barcelona kwa takribani
muongo mmoja sasa, akiwasaidia kutwaa makombe matatu ya ligi ya mabingwa
Ulaya, makombe sita ya La Liga na mengine kadhaa ambayo hayajatajwa.
Mourinho,
ambaye alimpoka taji la La Liga Guardiola mwaka 2012 wakati akiinoa
Real Madrid anahisi kuwa Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 27 ndio
nguzo kubwa ya mafanikio ya klabu hiyo
"Ndani
ya kipindi cha miaka 10 ambacho Messi hatokuwepo, ramani ya soka la
Ulaya lazima itabadilika sana," Mourinho aliiambia talkSPORT.
"Walichoshinda
Barcelona katika miaka kadhaa iliyopita wakiwa ama na Frank Rijkaard,
Pep Guardiola au Luis Enrique kama makocha ni kwa sababu wamekuwa na
kiumbe huyu."
Chelsea
wamewahi kuhusishwa na kumwania Messi, ambaye kwa wakati fulani
alionekana kutokuwa na furaha klabuni hapo, lakini Mourinho alikanusha
vikali taarifa hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni