STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 10 Juni 2015

FIFA KUAMUA TAREHE YA UCHAGUZI JULAI.

KASHFA nzito iliyolikumba Shirikisho la Soka Duniani-FIFA imefanya kuandaliwa mkutano wa kipekee wa kamati ya utendaji Julai mwaka huu kujadili tarehe ya uchaguzi kwa ajili ya kuziba nafasi ya rais Sepp Blatter alitangaza kuachia ngazi wiki iliyopita. 

Katika taarifa yake FIFA imedai kuwa hakuna muda rasmi ulioamuliwa mpaka kuelekea katika mkutano huo lakini wapekenyuzi wa mambo wanadai kuwa uchaguzi unaweza kufanyika Desemba 16 mwaka huu. 

Blatter alitangaza kujiuzulu wadhifa wake huo Jumanne iliyopita ikiwa zimepita siku nne toka alipochaguliwa tena kuliongoza shirikisho hilo jijini Zurich. Hata hivyo Blatter anataka kuendelea kushikilia madaraka hayo mpaka hapo mbadala wake atakapochaguliwa na anataka kuongoza nguvu ya kulisafisha shirikisho hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox