STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 10 Juni 2015

MOURINHO KUSAJILI WATATU KIANGAZI.

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho amesema kuwa jambo la kwanza muhimu katika usajili wa majira haya ya kiangazi in kuhakikisha anaendelea kubakia na wachezaji wake bora lakini ameahidi kusajili wengine watatu wapya. 

Baada ya Chelsea kunyakuwa taji la Ligi Kuu msimu wa 2014-2015, Mourinho raia wa Ureno anataka kuendelea wimbi lake la ushindi kea kufanya mabadiliko kidogo katika kikosi chake. 

Ingawa anataka kutafuta mbadala wa Didier Drogba anayeondoka na kutafuta wachezaji wengine wawili watakaoongeza ushindani katika baadhi ya nafasi katika kikosi chake, Mourinho pia amepania kupambana na mahasimu wake ambao watajaribu kununua nyota wake. 

Akihojiwa Mourinho amesema katika misimu mingine alifurahi sana kuuza baadhi ya wachezaji wake hata wale wazuri lakini mwaka huu hataki kabisa kufanya hivyo na hiyo ndio changamoto kubwa inayomkabili hivi sasa. 

Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kama ataweza kuwabakisha nyota wake kama Eden Hazard, Nemanja Matic, Branislav Ivanovic, Diego Coast na Cesc Frabregas anadhani atakuwa amefanikiwa lengo lake la kwanza. 

Mourinho amesema baada ya hapo atahitaji kununua wachezaji watatu, mshambuliaji atakayechukua nafasi ya Drogba, beki na kiungo ili kuongeza ushindani katika kikosi chake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox