STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 9 Juni 2015

MORATA AKANUSHA TETESI ZA KUREJEA MADRID.

MSHAMBULIAJI wa Juventus, Alvaro Morata amesema kurejea Real Madrid kutategemea watu wengi kufuatia taarifa kuwa klabu hiyo inaweza kumrejesha Santiago Bernabeu. 

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 alihamia jijini Turin mwaka jana ambako amefanikiwa kushinda taji la Serie A, Kombe la Italia huku akifunga bao katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kufungwa na Barcelona mabao 3-1. 

Akihojiwa kuhusiana na tetesi hizo Morata alikanusha kuwepo mazungumzo ya yeye kurejea Madrid kufuatia kuondoka kwa kocha Carlo Ancelotti na nafasi yake kuchukuliwa na Raf Benitez lakini hata hivyo hajafunga milango ya kuja kuichezea tena timu hiyo. 

Morata amesema hakuna yeyote aliyezungumza naye kuhusu suala hilo kwani ni kitu ambacho kinaweza kutegemea kuhusishwa kwa watu wengi. 

Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa anafurahia maisha ya Italia na ni matumaini yake msimu ujao atarejea akiwa imara zaidi ili aweze kuisaidia klabu yake hiyo kushinda mataji zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox