STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 9 Juni 2015

KASHFA NYINGINE ZA UFISADI KWA MAAFISA WA FIFA. HII SASA KALI

MAKAMU wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Jack Warner
amekumbwa na kashfa nyingine na uchunguzi dhidi yake unafanyika kuhusiana na kupotea kwa fedha ambazo zililengwa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti mwaka 2010. 

Warner aliitembelea nchi hiyo miezi kadhaa baada ya tetemeko hilo na kuchangisha kiasi cha dola 750,000 kutoka FIFA na Shirikisho la Soka la Korea Kusini kwa ajili ya kuijenga upya nchi hiyo. 

Lakini hata hivyo, Wachunguzi wa kashfa hiyo ya rushwa inayoikabili FIFA wanasema fedha hizo zilihamishwa katika akaunti inayomilikiwa na Warner kwa ajili ya matumizi yake binafsi. 

Miaka minne baadaye fedha hizo bado hazijatolewa maelezo huku Warner mwenyewe amekana tuhuma zote zilizotolewa dhidi yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox