Haendi popote: Walcott ataendelea kubaki Arsenal mpaka mwaka 2019
Theo Walcott amekubali kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal.
Nyota huyo wa Uingereza (26), alikuwa anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na 'The Gunners'.
Lakini baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati yake na viongozi wakuu wa klabu ya Arsenal, dili hilo sasa lianenda kukamilika.
Dili
hilo litambakisha Walcott klabuni hapo mpaka mwaka 2019 na kumfanya
alipwe kiasi cha mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki na kuwa moja ya
wachezaji wa Arsenal wanaolipwa pesa ndefu zaidi.
Arsenal
watathibitisha rasmi makubaliaono hayo wiki mbili zijazo, pengine kabla
ya kuanza kwa msimu mpya wa EPL, ambapo watafungua dimba wakiwa
nyumbani Emirates na klabu ya West Ham.
Olivier Giroud:yupo katika wakati mgumu baada ya Walcot kuonesha njaa na nafasi yake ya mshambuliaji wa kati.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni