Di Maria amewaambia Man United anataka kujiunga na PSG
Stoo
ya United ikiwa na maski za Robin van Persie, Di Maria na Radamel
Falcao ambazo ndizo pekee zinazouzwa kwa bei rahisi kabisa.
Angel
di Maria amewaambia Manchester United kwamba anataka kuhamia kunako
klabu ya Paris Saint-Germain -huku Laurent Blanc akisisitiza kuwa na nia
ya kunasa Muargentia huyo hata ikibidi wiki hii.
Mabingwa
hao wa Ufaransa, awali walitoa ofa ya pauni milioni 46.5 na inasemekana
kuwa mpaka kufikia siku ya Jumatatu dili hilo litakuwa limekamilika.
Kocha
wa Manchester United aliwaambia wachezaji wake mapema kabisa kabla ya
mchezo dhidi ya Barcelona kwamba Di Maria yuko mbioni kujiunga na PSG
baada ya kukacha kujiunga na wenzake kwa ajili ya mchezo huo huko Santa
Clara.
Marcos
Rojo kwa upande wake hakuwepo pia lakini yeye taarifa zake ziko wazi
kwamba ana matatizo katika pasi yake ya kusafiria lakini hata hivyo
anaweza kukumbana na hatua za kinidhamu kutoka kwa kocha wake kutokana
na uzembe huo.
Huku
PSG wakijianda kukipiga na Man United siku ya Jumatano huko Chicago,
Blanc amesema kwamba: 'Bila shaka ni mchezaji mzuri. hakuna chochote
kilichothibitishwa mpaka sasa. Bado kuna mkanganyiko kwamba atakuja hapa
U.S. Je, ni jezi ipi anavaa, sisi hatujui.
Kama atafanya chaguo lake
mwenyewe kuhusu mahali pa kwenda, basi naamini iakuwa ni PSG.'
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni