De Bruyne alipata kura 367 huku Robben akipata kura 94 na Neuer
akipata kura 67. Kumbuka msimu uliopita Mbelgiji huyu alifunga magoli 10 huku akitoa assists 20, bila shaka huu ulikuwa msimu mzuri sana kwa kijana huyu ambaye kwa sasa anahusishwa kuhamia pale Etihad…
Kutokana na kutopata nafasi katika klabu yake ya zamani ya Chelsea, De Bruyne alienda Wolfsburg ambapo ameiwezesha timu hii kumaliza nyuma ya bingwa Bayern Munich huku akiisaidia timu yake kutwaa kombe la DFB-Pokal.
Pia kocha wa Wolfsburg Dieter Hecking alitajwa kama kocha bora wa
msimu baada ya kukusanya kura 203. Makocha wengine kama Markus
Weinzierl wa Augsburg, Lucien Favre, Jurgen Klopp na Pep Gurdiola
walimaliza nyuma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni