ALIYEKUWA kipa namba moja wa Arsenal, Wojciech Szscesny amesema anakwenda AS Roma ya Italia kwa mkopo wa muda mrefu.
Mlinda
mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 ameposti video katika akaunti yake
ya Instagram jana jioni akithibitisha ataondoka Emirates kuhamia Rome. "Habari za jioni Giallorossi! Nina furaha sana, kwa sababu ninakwenda Roma kesho. Tutaonana hivi karibuni,".
Szczesny amelazimika kuondoka The Guunners baada ya koch Arsene Wenger kumsajili Petr CVech kutoka Chelsea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni