KOCHA wa timu ya taifa ya Argentina, Gerardo Martino amesema kikosi chake kilikosa bahati kufuatia kupoteza mchezo wao wa fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya Chile jana na kudai yuko nyuma akiwaunga mkono wachezaji wake. Argentina walilikosa taji hilo baada ya kupoteza mchezo huo kwa wenyeji Chile kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida na ule wa nyongeza. Akihojiwa Martino amesema hawakucheza vile walivyozoea na hata wapinzani wao pia kwa timu hizo mbili zilifanikiwa kwa kiasi kikubwa ya kupunguza kasi ya mwenzake. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kutokana na hilo sio kikosi chake au Chile waliotengeneza nafasi za kutosha kwa ajili ya kufunga. Hiyo inakuwa mara ya pili kwa Argentina kunyang’anywa tonge mdomoni kwa miezi 12 iliyopita walijikuta wakitoka vichwa chini baada ya kufungwa na Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Mara ya mwisho Argentina kunyakuwa taji kubwa la kimataifa ilikuwa miaka 22 iliyopita na sasa inaonekana itabidi waendelee kuvumilia zaidi ili kukata kiu yao hiyo.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumapili, 5 Julai 2015
Home
/
Unlabelled
/
KOCHA WA ARGENTINA ADAI BAHATI HAIKUWA UPANDE WAO BAADA YA KULIKOSA TAJI LA COPA AMERICA.

About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni