BONDIA
Floyd Mayweather amepokonywa mkanda wa WBO uzito wa Welter alioshinda
dhidi ya Manny Pacquiao- na Anthony Mundine ameomba kuzichapa naye
Septemba.
Mayweather
alishindwa kulipa wakati Ijumaa dola za KImarekani 200,000 ambayo ni
ada ya mkanda kwa WBO na Kamati imeamua kumvua taji hilo mbabe huyo
mwenye umri wa miaka 38. Inamaanisha Timothy Bradley JR anatarajiwa
kuvikwa mkanda huo baada ya kumshinda kwa utata Jessie Vargas mwezi
uliopita.
Mayweather bado ana siku 14 za kukata rufaa, ingawa uamuzi hautarajiwi kubadilishwa.
"Kamati
ya ubingwa wa dunia ya WBO imeona hakuna namna nyingine zaidi ya
kuendelea kumtambua Floyd Mayweather Jr. kama bingwa wa WBO uzito wa
Welter duniani na kumvua mkanda kwa kushindwa kutimiza raratibu za
mapambano ya ubingwa wa dunia wa WBO," imesema WBO Jumatatu.
Mayweather
bado ni bingwa wa uzito wa Welter ma Super Welter wa WBC na WBA, ingawa
mabondia hawaruhusiwi kushikilia mataji ya uzito tofauti.
Mayweather
anatarajiwa kurejea ulingoni kwa mara ya 49 ambalo linaweza kuwa
pambano lake la mwisho Septemba na Mundine – mshindani mkuu wa WBC
katika uzito wa Super-Welter amemuandikia barua ya wazi bondia huyo
kuomba awe mpinzani wake afuataye.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni