Washambuliaji wawili wakongwe, Hamis Kiiza na Mussa Hassan Mgosi wameonyesha ukubwa dawa baada ya kuingoza Simba kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Kombaini ya Zanzibar kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo.
Mechi hiyo ni ya kwanza kwa Simba ambayo imecheza chini ya Kocha Dylan Kerr raia wa Uingereza aliyejiunga na Simba kuchukua nafasi ya Goran Kopunovic raia wa Serbia.
Licha ya mechi kuwa kali, Simba ilicheza taratibu katika kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Kerr alibadilisha karibu timu yote na baada ya hapo Simba ilicheza kwa kasi na kuwafanya mashabikiw ake waliokuwa uwanjani hapo kushangilia kwa nguvu.
Ushindi huo unaifanya Simba kuanza vizuri kwa maana ya mechi za kirafiki kwa kuwa imekuwa ikiweka kambi tu za mazoezi kuanzia Lushoto mkoani Tanga kabla ya kutua Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni