Mkurugenzi
wa Arsenal, Lord Harris amemsapoti Arsene Wenger kuvunja rekodi ya
usajili ya klabu kwa kupata saini ya mshambuliaji wa kati wa maana
majira haya ya kiangazi.
Harris amesema Wenger anaweza kusajili straika yeyote isipokuwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Karim
Benzema ndiye mshambuliaji aliyepo kwenye rada za Wenger na Lor Harris
anayesimamia masuala ya fedha, amemhakikishia Mfaransa huyo kwamba kuna
paundi milioni 200 kwenye akaunti, hivyo alete watu wa maana.
Mkurugenzi
huyo amekiri kuwa awali ujenzi wa uwanja wa Emirates uliwafanya
wasitumie fedha nyingi kweye usajili, lakini sasa umefika wakati wa
kuwekeza katika usajili wa wachezaji watakaowapa uwezo wa kushindana
barani Ulaya.
"Pesa
ilibana tulipohamia Emirates, lakini sasa ipo ya kutosha," Amesema
Harris. "Tunaweza kwenda sokoni na kununua mchezaji yeyote isipokuwa
wale wasionunulika.
Katika akaunti tuna paundi milioni 200, tumemwambia
Wenger asiwe na shaka, tunaweza kumpa paundi milioni 100 na lazima
azitumie".
"Kwa
wakati huu hatuna mpango wa kusajili mchezaji yeyote, vinginevyo
apatikane nyota kama Mesut Ozil au Alex Sanchez. Kwasasa kocha
anatafuta, lakini hawapatikani. Tunaweza kuvunja rekodi ya klabu ya
usajili, mbali na Messi na Ronaaldo, Wenger anaweza kusajili yeyote".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni