MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ubelgiji, Christian Benteke amesema kwamba ametua Liverpool kutoka Aston Villa ili kushinda mataji.
Benteke,
aliyejiunga na timu ya Midlands mwaka 2012 na kuifungia mabao 42 katika
mechi 88 za ligi, arrived aliwasili viwanja vya mazoezi vya Wekundu
hao, Melwood Jumatano baada ya Liverpool kukamilisha uhamisho wake wa
Pauni Milioni 32.5.
Liverpool
pia imewasajili washambuliaji Danny Ings kutoka Burnley, na Roberto
Firmino kutoka Hoffenheim, ili kuirejeshea makali safu yao ya
ushambuliaji inayomkosa wa muda mrefu, Daniel Sturridge na Luis Suarez
aliyehamia Barcelona msimu uliopita na Raheem Sterling aliyetimkia
Manchester City.
Akizungumza mara baada ya kukamilisha uhamisho wake, Benteke alisema; "NIna furaha sana kuwa hapa na ningependa kumshukuru mmiliki, Ian (Ayre) na pia kocha kwa jitihada zao za kunifikisha hapa.
"Nafikiri ilikuwa klabu sahihi, kwa sababu nilikuwa nina mawasiliano mazuri na kocha na nilitaka kuwa sehemu ya mipango yake.
"Nafahamu
Liverpool ni habari kubwa. Wameshinda mataji mengi ya Ligi Kuu na
matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia Kombe la UEFA na mataji mengi.
Nafahamu ni klabu kubwa.
Alipoulizwa
ni kipi kinamhamasisha yeye kama mchezaji, alisema: "Ni juu ya kushinda
mataji. Ni kuhusu kufanya kitu fulani katika kazi yangu ambacho naweza
labda kuwaeleza wanangu nilichokifanya,".
WAPYA WALIOSAJILIWA LIVERPOOL 2015
Christian Benteke - Pauni Milioni 32.5 kutoka Aston Villa
Roberto Firmino - Pauni Milioni 29 kutoka Hoffenheim
Nathaniel Clyne - Pauni Milioni 12.5 kutoka Southampton
Joe Gomez - Pauni Milioni 3.5 kutoka Charlton
Danny Ings kutoka Burnley
James Milner kutoka Manchester City
Adam Bogdan kutoka Bolton
JUMLA IMETUMIA:
Pauni Milioni 77.5
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni