Nyota namba tatu kwa ubora wa mchezo wa tenesi muingereza Andy Murray ametwaa ubingwa wa michuano ya Rogers
Murray
ametwaa ubingwa huu baada ya kumshinda mpinzani wake Novack Djokovic
kwa seti 6-4 4-6 6-3 katika mchezo uliochukua muda wa saa tatu.
Kwa ushindi huu Murray anavunja mwiko wa kupoteza mapambano manane dhidi ya Novack ambae anashilikia nafasi ya kwanza kwa ubora.
Murray amemzawadia ushindi huo kocha wake Amelie Mauresmo,aliyepata mtoto wa kiume siku ya jumapili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni