Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu England Timu ya Chelsea, leo imepata ushindi wake wa kwanza msimu kwenye ligi hiyo baada ya kuichapa kwa mbinde timu ngumu ya West Bromwich Albion kwa mabao 3-2Kiungo mpya aliyekaribia kutua Man United Pedro amekuwa mchezaji bora wa mechi katika mchezo wake wa kwanza na timu hiyo ya darajan baada ya kutoa pasi ya goli lililofungwa na Diego Costa dakika ya 30, na akifunga bao la kwanza kwenye dakika ya 20 wakati lile la ushindi likifungwa na beki Cesar Aziplicueta dakika ya 43
Katika mchezo huo kapten wa Chelsea John Terry litolewa nje kwenye dakika ya 55 baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa WBA ambayo pia timu hiyo ikijutia penalti iliyookolewa na kipa wa Chelsea Thibaut Courtious
Licha ya kukosa mkwaju Morrison aliifungia bao WBA dakika ya 36 na 46, na kuifanya timu hiyo kushuka mkiani mwa ligi hiyo huku Chelsea wao wakipanda mpaka nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi hiyo ngumu duniani


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni