Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alsiema kuwa kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakidhi vifaa mbalimbali vy a ligi ambavyo ni jezi za kawaida, jezi za mechi, viatu na vifaa vingine vinayohitajika.
“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwaa tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki lii zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya 2015/2016” Alisema Twissa.
Twissa alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata buruddaniya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka sekta hii.
Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiri katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanza ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa” Alisema Twissa.
Wawakilishi wa kionyesha jezi za Mtibwa Sugar, (picha na michuzi blog) |
“Ninatoa mwito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa” alisema.
Aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sharia kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya madhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika mapema pia timu zitakazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.
Wawakilishi wa Kagera Sugar wakionyesha jezi za nyumbani na ugenini za timu hiyo (picha na michuzi blog) |
Wakionyesha jezi za Coastal union za nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
Jezi za Mtibwa Sugar nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
Jezi za Yanga nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
Jezi za Simba SC za nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
Jezi za Stand United za ugenini na nyumbani |
Picha ya Pamoja katika utoaji wa vifaa vya michezo kwa vilabu |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni