MASHABIKI wa Arsenal wameitaka klabu hiyo kupitia upya na kufanya marekebisho ya sera zao kufuatia kufanyika kwa usajili wa golikipa Petr Cech pekee katika usajili wa majira ya kiangazi ambao dirisha lake lilifungwa jana.
Cech alitua Emirates kwa kitita cha paundi milioni 10 na kuwa mchezaji pekee aliyesajiliwa na timu hiyo pamoja na kuhitaji kuimarisha nafasi kadhaa katika sehemu ya kiungo na ushambuliaji.
Ukimya waliokuwa nao katika dirisha la usajili hakutokana kwasababu ya fedha kwani mkrugenzi wa Arsenal, Philip Harris aliwahi kukaririwa akidai kuwa klabu hiyo inaweza kusajili mchezaji yeyote duniani kasoro Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Mashabiki hao wa Arsenal wamesema klabu yao iko vizuri kiuchumi na wasikitika kwa kushindwa kwao kufanya usajili zaidi mpaka dirisha li,efungwa.
Taarifa ya mashabiki hao iliendelea kudai kuwa Arsenal imejenga kikosi imara na nyongeza ya mchezaji mmoja au wawili ingeimarisha zaidi nafasi ya kunyakuwa taji la Ligi Kuu msimu huu.
Taarifa imesema wakati umefika wa Arsenal kubadili sera zake na kuhakikisha wanasajili wachezaji zaidi wa kiwago cha juu kwani sasa hivi hawana matatizo ya kifedha kama ilivyokuwa huko nyuma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni