STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 22 Oktoba 2015

AZAM JINO KWA JINO NA YANGA KILELENI, TEGETE KAMA MAGURI, MTIBWA YABANWA, ANGALIA MATOKEO YOTE YA LEO



Goli pekee la beki wa Azam FC Shomar Kapombe lilitosha kuipatia Azam FC pointi tatu muhimu mbele ya Ndanda FC katika mwendelezo wa ligi kuu ya vodacom.



Katika mchezo huo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Azam FC waliuanza mchezo taratibu huku wakitumia zaidi mipira mirefu katika kusaka ushindi katika mchezo wa leo.

Ndanda FC muda mwingi walikuwa nyuma na kumuacha Atupele Green pekee yake mbele ambapo katika dakika 45 za mwanzo Ndanda FC walifanikiwa kutengeneza nafasi moja ambapo Azam FC walitengeneza nafasi 5.

Katika dakika ya 7 nusura Ame Ally aiiandikie goli la kuongoza Azam FC baada ya kupokea pasi ndefu ya Franky Domayo na kushindwa kumchambua kipa wa Ndanda FC Jackson Chove.

Dakika 3 baadae Ame Ally alishindwa tena kutumia vyema krosi ya Kipre Tcheche ambapo kichwa chake kilipaa juu ya lango.

Kipre Tcheche jitihada zake za kuipatia goli Azam FC ziliishia kwa Chove ambapo leo aliokoa hatari nyingi na kupelekea timu yake isifungwe idadi kubwa ya Magoli.

Kosa kosa za Azam FC ziliendelea kipindi cha pili na hata alipoingia John Bocco kuchukuwa nafasi ya Ramadhan Singano ali ilendelea kuwa ile ile.

Katika kipindi cha Ndanda FC nao walijaribu kutengeneza nafasi kadhaa lakini uimara wa Mwadin Ally na safu yake ya ulinzi iliitoa salama Azam FC hii leo.

Katika dakika ya 79 baada ya kosa kosa Kipre Tcheche alipiga krosi iliyo ungwa na Shomari Kapombe na kuiandikia Azam FC goli ambalo lilidumu kwa dakika zote 90.

Matokeo ya leo Azam FC wanaendele kukipizana na Yanga SC katika usukani wa ligi kuu ya codacom.
Na kule shinyanga
Mshambuliaji Jerry Tegete ameiongoza Mwadui FC kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ngumu ya Mgambo FC.

Mgambo waliosafiri hadi Mwadui Complex mkoani Shinyanga walikubali kipigo hicho huku Tegete akitupia mabao mawili. Bao jingine lilifungwa na Malika Ndeule.

Bao hilo linakuwa la tatu ndani ya mechi mbili kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga ambaye anaonekana kurejea katika kiwango chake.


Ushindi huo umeipa Mwadui nafasi ya kufikisha pointi 14 na kusogea hadi nafasi ya 6 ikiishusha Prisons ya Mbeya.

Kule jijini Mbeya
Mshambuliaji  wa Mbeya city Geofrey Mlawa leo amiiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya African Sport katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Goli hilo la Geofrey Mlawa lilipatikana katika dakika ya 12 ya kipindi cha kwanza na kudumu kwa dakika zote 78 zilizosalia na kuipa point tatu muhimu Mbeya city.

Ushindi huo ni wa pili kwa Mbeya city msimu huu ambapo wamepoteza michezo mitano na kutoa sare mchezo mmoja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox