STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 21 Novemba 2015

Kavumbagu aimaliza Zanzibar kombe la Chalenji, yaanza kwa kichapo

Zanzibar
Timu ya Zanzibar leo imeianza vibaya michuano ya kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na kati baada ya kulambishwa bao 1-0 na timu ya taifa ya Burundi.

Katika mchezo huo mkali wa ufunguzi wa michuano hiyo jijini Addis Ababa, Ethiopia, washindi Burundi walipata bao la pekee na la ushindi kupitia kwa mshambuliaji wa Azam, Didier Kavumbagu kwa kombora kali mnamo dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza.

Zanzibar itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kukosa nafasi ya wazi kupitia kwa Mudathir Yahya aliyeipasha shuti lake akiwa ndani ya kumi na nane baada ya kumegewa pasi nzuri kutoka kwa Ame Ali.
Hata hivyo, Burundi nao walikosa nao la pili baada ya mshambuliaji anayewaniwa na Simba, Laudit Mavugo kumpa pasi nzuri Kavumbagu lakini mfungaji huyo wa bao la kwanza akapaisha mpira wa kichwa sentimita chache juu ya lango la Zanzibar.

Zanzibar: Mwadini Ali Mwadini (GK), Haroub Ali Nadir, Masoud Said Nassoro, Haji Mwinyi Ngwali, Issa Haidar Dali, Yahya Abbas Mudathir, Suleiman Kassim Suleiman, Khamis Micha Khamis, Awadh Juma Issa, Ame Ali Amour ( Hamad Ibrahim 83′), Mohammed Abdrahman Mohammed

Burundi: Arthur Arakaza, Karim Nzigyimana, Fataki Kiza, David Nshimirana, Issa Hakizimana, Yusuf Ndikumana, Fuadi Ndayienga, Cedric Amisi, Shassir Nahimana, Didier Kavumbagu, Laudit Mavugo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox