STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 19 Novemba 2015

MECHI ZA CHAMPIONS LEAGUE NA EUROPA LEAGUE KAMA KAWAIDA

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA, limebainisha kuwa mechi zake za Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League zitaendelea kama zilivypangwa wiki ijayo. 
 
Ratiba ya michezo mingi ilisimamishwa au kusogezwa mbele maeneo mengi ya Ulaya kufuatia mashambulio ya kigaidi yaliyofanyika jijini Paris Ijumaa iliyopita. 
 
Mchezo wa kirafiki kati ya Ujerumani na Uholanzi uliokuwa uchezwe jijini Hannover Jumanne nao ulifutwa dakika za mwisho baada ya taarifa za kuwepo kwa tishio la bomu. 
 
Msemaji wa UEFA amesema shirikisho hilo linafanya kazi kwa karibu na klabu zitakazokuwa nyumbani pamoja na mamlaka husika ili kuhakikisha taratibu muhimu zinafuatwa kuhakikisha usalama wa watu wote. 
 
Msemaji huyo aliendelea kudai kuwa bado hawajalijadili suala la mashabiki watakaosafiri kwani hilo linahusu mamlaka husika kutoa maamuzi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox