STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 23 Novemba 2015

REKODI YA KIPEKEE YA AGUERO EPL..........


Kipigo cha jumamosi iliyopita kutoka kwa Liverpool ni kitu ambacho watu wengi katika klabu ya Manchester City hawakutaraji,  lakini ilikuwa ni siku ya kumbukumbu nzuri kwa mmoja wa wachezaji wa Manuel Pellegrini. 

  Goli la Sergio Aguero katika dimba la Etihad vs Liverpool lilimfanya atimize jumla ya magoli 7 katika mechi 9 za Premier League msimu huu. 
 
  Goli hilo pia alilofunga katika dakika ya 44 likamfanya mshambuliaji huyo kuwa mwanasoka mwenye asili ya Amerika ya kusini ambaye anaongoza kwa kufunga magoli mengi zaidi katika ligi kuu ya Uingereza. 
 

Mshambuliaji huyo mwenye umri miaka 27, sasa ana magoli 85 katika EPL – goli moja zaidi ya muargentina mwenzie Carlos Tevez ambaye wakati akivichezea vilabu vya West Ham, Man United na Man City alifanikiwa kufinga magoli 84.
 

Luis Suarez ni watatu kwenye listi hiyo akiwa na magoli 69 aliyoyafunga katika misimu mitatu na nusu aliyoichezea Liverpool kabla ya kuhamia FC Barcelona 2014.
 
Mruguay mwenzie Suarez, Gus poyet anashika nafasi ya 4 katika kidti hiyo akiwa na magoli 54 aliyoyafunga wakati akiwa katika safu ya kiungo ya vilabu vya Chelsea Na Tottenham. 
 
 Nolberto Solano anakamilisha listi ya tano ya wafungaji bora wa muda wote wa kutoka America ya kusini katika EPL – Solano alivitumikia vilabu vya Newcastle, Aston Villa na West Ham.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox