STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 9 Desemba 2015

MATOKEO YA UEFA PAMOJA NA TIMU ZILIZOFUDHU 16 BORA......................

  Chelsea 2-0 Porto: Pressure lifted as Jose Mourinho's men march into the Champions League
 
MATOKEO LIGI YA MABINGWA ULAYA
Desemba 9, 2015  
 
KAA Gent 2-1 Zenit St Petersburg
Roma 0-0 BATE Borisov
Dynamo Kyiv 1-0 Maccabi Tel Aviv
Olympiakos 0-3 Arsenal
Bayer 04 Leverkusen 1-1 Barcelona
Valencia CF 0-2 Lyon
Chelsea 2-0 FC Porto
Dinamo Zagreb 0-2 FC Bayern Munich
 
Giroud akishangilia baada ya kuifungia Arsenal mabao yote matatu 
MSHAMBULIAJI Olivier Giroud usiku huu ameibuka shujaa baada ya kufunga mabao yote matatu, Arsenal ikishinda 3-0 ugenini dhidi ya wenyeji Olympiakos katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Georgios Karaiskakis, Giroud alifunga mabao hayo dakika za 29, 49 na 67 kwa penalti na kuifanya The Gunners kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo kwa kufikisha pointi tisa, nyuma ya Bayern Munich iliyomaliza na pointi 15.
 
Lakini Arsenal inafuzu hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa kwa wastani wa mabao tu, kwani imefungana kwa pointi na Olympiakos iliyoishia nafasi ya tatu.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Bayern Munich imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Dinamo Zagreb, mabao yote akifunga Robert Lewandowski dakika ya 61 na 64 Uwanja wa Maksimir.

Willian akishangilia baada ya kuifungia Chelsea katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Porto

Chelsea nayo imekuwa timu ya tatu ya England kwenda 16 Bora ya michuano hiyo baada ya Manchester City na Arsenal, kufuatia ushindi wa mabao 2-0  dhidi ya FC Porto Uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo wa Kundi G.
 
Ivan Marcano Sierra alijifunga dakika ya 12 kuipatia The Blues bao la kwanza kabla ya Willian Borges Da Silva kufunga la pili dakika ya 52.
 
Mchezo mwingine wa kudi hilo, Dynamo Kyiv imeshinda 1-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv, bao pekee la Denys Garmash dakika ya 16 Uwanja wa Olimpiki.
 
Chelsea inamaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi zake 13, ikifuatiwa Kyiv pointi 11, Porto pointi 10 na Maccabi ambayo haina pointi. 
 
Katika mchezo wa Kundi E, Barcelona imelazimishwa sare ya 1-1 na Bayer 04 Leverkusen iliyoanza kupata bao kupitia kwa Javier Hernandez ‘Chicharito’ dakika ya 23, kabla ya  Lionel Messi kuwasawazishia mabingwa hao watetezi dakika ya 20 Uwanja wa BayArena.
 
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Roma imetoka 0-0 na BATE Borisov Uwanja wa Olimpico. Barca inamaliza kileleni kwa pointi zake 14, ikifuatiwa na Roma pointi sita na sawa na Bayer 04 Leverkusen, wakati imeshika mkia kwa pointi zake tano.
Valencia CF imefungwa 2-0 nyumbani na Lyon ua Ufaransa katika mchezo wa Kundi H.
 
Katika mchezo huo uliofanyika Uwa ja wa Mestalla, mabao ya wageni yamefungwa na Maxwell Cornet dakika ya 37 Alexandre Lacazette dakika ya 76.
 
Mchezo mwingine wa kundi hilo, KAA Gent imeshinda 2-1 dhidi ya Zenit St Petersburg mabao yake yakifungwa na Laurent Depoitre dakika ya 18 na Danijel Milicevic dakika ya 78, huku la wageni likifungwa na Artem Dzyuba dakika ya 65 Uwanja wa Ghelamco Arena. 
 
Timu zilizofuzu 16 Bora ni Real Madrid, Paris Saint-Germain, VfL Wolfsburg, PSV, Atletico Madrid, Benfica, Manchester City, Juventus, Barcelona, Roma, FC Bayern Munich, Arsenal, Chelsea, Dynamo Kyiv, Zenit St Petersburg na KAA Gent.
 Olympiacos 0-3 Arsenal: Olivier Giroud's superb hat-trick seals Champions League last-16
Zifuatazo ndiyo timu 16 zilizovuka kutoka hatua ya makundi, yaani timu mbili kutoka kila kundi.
Champions League draw guide: Time, dates of fixtures, teams and seedings
England imefanikiwa kuingiza timu tatu kama ilivyo kwa Hispania na kufuatiwa na Ujerumani  timu mbili pamoja na Italia.

Kundi A - Real Madrid (kinara), Paris Saint-Germain (nafasi ya pili)
Kundi B - Wolfsburg (kinara), PSV Eindhoven (nafasi ya pili)
Kundi C - Atletico Madrid (kinara), Benfica (nafasi ya pili)
Kundi D - Manchester City (kinara), Juventus (nafasi ya pili)
Kundi E - Barcelona (kinara), Roma (nafasi ya pili)
Kundi F - Bayern Munich (kinara), Arsenal (nafasi ya pili)
Kundi G - Chelsea (kinara), Dynamo Kyiv (nafasi ya pili)

Kundi H - Zenit (kinara), Gent (nafasi ya pili)

 The 16 sides who have progressed to the first knockout stage will be hoping to get their hands on this trophy

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox