STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 14 Desemba 2015

SAMATA AINGIA 3 BORA YA MCHEZAJI BORA WA AFRICA, ORODHA YOTE IKO HAPA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameingia tatu bora ya Tuzo ya Mwanasoka Bora Nayecheza Afrika.
 
Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika  imesema Samatta ameingia fainali na kipa Robert Kidiaba anayecheza naye TP Mazembe ya DRC na Baghdad Boundjah wa Algeria na Etoile du Sahel ya Tunisa.
 
Katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa Jumla wa Afrika, walioingia fainali ni Andre Ayew wa Ghana na Swansea City, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund na Yaya Toure wa Ivory Coast na Manchester City, anayeshikilia tuzo hiyo.

 
Majina hayo yametangazwa mchana wa leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Abuja, Nigeria na washindi wapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na makocha wakuu wa timu za taifa au Wakurugenzi wa Ufundi wa Vyama na mashirikisho ya soka ya nchi zote wanachama wa CAF.
 
Washindi watatangazwa katika usiku wa tuzo za Glo-CAF Januari 7 mwaka 2016.


Mchezaji wa Kike wa Mwaka
·         Gabrielle Onguene, Cameroon
·         Gaelle Enganamouit, Cameroon
·         Ngozi Ebere, Nigeria
·         N'rehy Tia Ines, Ivory Coast
·         Portia Boakye, Ghana
Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka  
·         Adama Traore, Mali
·         Kelechi Nwakali, Nigeria
·         Samuel Diarra, Mali
·         Victor Osimhen, Nigeria
·         Yaw Yeboah, Ghana
Chipukizi Mwenye Kipaji Zaidi       
·         Azubuike Okechukwu, Nigeria
·         Etebo Oghenekaro, Nigeria
·         Djigui Diarra, Mali
·         Mahmoud Abdelmonem ‘Kahraba’, Misri
·         Zinedine Ferhat, Algeria
Kocha wa Mwaka 
·         Baye Ba, Mali, U17
·         Emmanuel Amunike, Nigeria U17
·         Fawzi Benzarti, Etoile Sportive de Sahel
·         Hervé Renard, Ivory Coast
·         Patrice Carteron, TP Mazembe
Refa wa Mwaka
·         Alioum, Cameroon
·         Bakary Papa GASSAMA, Gambia
·         Eric Arnaud OTOGO CASTANE, Gabon
·         Ghead Zaglol GRISHA, Misri
·         Janny SIKAZWE, Zambia
Gwiji wa Afrika
·         Charles Kumi Gyamfi, Ghana
·         Samuel Mbappe Leppe, Cameroon
Timu ya Taifa ya Mwaka
·         Ivory Coast
·         Ghana
·         Mali U17
·         Nigeria U17
·         Nigeria  U-23
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka
·         Ghana
·         Cameroon
·         Afrika Kusini
·         Zimbabwe
Klabu ya Mwaka
·         USM Algers , Algeria
·         TP Mazembe, DRC
·         Orlando Pirates, Afrika Kusini
·         Etoile Sportive du Sahel, Tunisia


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox