Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amewaomba mashabiki, wanachama na viongozi wa klabu hiyo kongwe nchini kumsamehe.
Niyonzima raia wa Rwanda amewambia kama aliwakosea, anaowamba wamwie radhi.
“Kama mtoto akikosea lazima arudi na kuoma msamaha, ninaomba radhi kama niliwakwaza kwa kila kilichotokea,” alisema Niyonzima.
Akizungumza kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga mtaa wa Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam, kiungo huyo wa zamani wa APR ya Rwanda alisisitiza kwamba ataendelea kuitumikia klabu yake kwa juhudi zote.
"Bado nina kiu ya kuitumikia Yanga kwa juhudi zote, najua mimi ni sehemu ya Yanga, ninatamani kurudi na kushirikiana na wenzangu kuendelea kupambana kwa ajili ya Yanga.
Akizungumza kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga mtaa wa Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam, kiungo huyo wa zamani wa APR ya Rwanda alisisitiza kwamba ataendelea kuitumikia klabu yake kwa juhudi zote.
"Bado nina kiu ya kuitumikia Yanga kwa juhudi zote, najua mimi ni sehemu ya Yanga, ninatamani kurudi na kushirikiana na wenzangu kuendelea kupambana kwa ajili ya Yanga.
Aidha,
Niyonzima amesema kwamba kulitokea kutoelewana kimawasiliano na ofisi
ya Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha kiasi cha kulifikisha suala hilo
kwenye hatua hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amesema kwamba suala la Niyonzima limefika katika uongozi mkuu wa klabu na lipo katika hatua nzuri.
Ingawa Muro hakuweza wazi, lakini inavyoonekana muda si mrefu Yanga itatangaza kuzika tofauti zake na mchezaji huyo na kumrejesha kundini rasmi.
Yanga
SC ilitangaza kuvunja Mkataba na Niyonzima, baada ya kuchelewa kurejea
klabuni kufuatia kuruhusiwa kwenda kuichezea Rwanda katika Kombe la
Mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA Challenge nchini Ethiopia Novemba.
Awali,
Yanga SC ilimsimamisha kwa muda usiojulikana Niyonzima kabla ya suala
lake kupelekwa Kamati ya Nidhamu, ambayo hatimaye ilichukua maamuzi
magumu.
Ulibaini plasta gumu (PoP) alilofunga baada ya kurejea akiwa amechelewa ilikuwa ni ‘geresha’ na vielelezo vingine alivyowasilisha vilikuwa ‘feki’ pia.
Na ikamnasa kwenye picha za video siku za karibuni ‘akijirusha’ sehemu mbalimbali za starehe ikiwemo kwenye onyesho la mwanamuziki Ali Kiba.
Haruna aliyezaliwa Februari 5, mwaka 1990 Gisenyi nchini Rwanda, alijiunga na Yanga SC mwaka 2011 akitokea APR ya kwao, ambako aliwasili mwaka 2007 akitokea Rayon aliyoichezea kwa misimu miwili baada ya kujiunga nayo akitokea Etincelles iliyomuibua mwaka 2005.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni