BAO pekee la mshambuliaji Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’
limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda, Kiiza aliifungia Simba SC bao hilo dakika ya tano tu kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya Ibrahim Hajib kutoka upande wa kushoto.
Na sasa Simba SC inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 14, ikiendelea kukaa nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC pointi 32 za mechi 13 na vinara, Azam FC pointi 35 za mechi 13 pia.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Emery
Nimubona, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Justice
Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Ibrahim Hajib/Danny Lyanga dk64, Hamisi
Kiiza/Awadh Juma dk89 na Peter Mwalyanzi/Said Ndemla dk31.
Mtibwa Sugar; Said Mohamed, Ally Shomary, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Salim Mbonde, Henry Joseph, Shaaban Nditi, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Hussein Javu/Jaffar Kibaya dk64, Ibrahim Rajab ‘Jeba’ na Mohammed Ibrahim/Vincent Barnabas dk64.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Prisons imeifunga Toto 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Stand United imeifunga 1-0 Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mbeya City imeifunga 1-0 Mwadui FC Uwanja wa Sokoine Mbeya, na katika uwanja wa CCM Mkwakwani ulimalizika kwa Coastal union kutoka sare ya goli 1-1 na Majimaji ya Songea, magoli yakifungwa na Dany Mrwanda na Abasalim Chedebel..
MATOKEO YOTE YA LEO
Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar
JKT Ruvu 1-5 Mgambo JKT
Toto Africans 0-1 Prisons
Stand United 1-0 Kagera Sugar
Mbeya City 1-0 Mwadui FC
Coastal Union 1-1 Majimaji
JKT Ruvu 1-5 Mgambo JKT
Toto Africans 0-1 Prisons
Stand United 1-0 Kagera Sugar
Mbeya City 1-0 Mwadui FC
Coastal Union 1-1 Majimaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni