Al-ahly wakicheza soka la taratibu na pasi fupi fupi walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Amri Gamal katika dakika ya 11 ya mchezo
Kuingia kwa goli hilo yanga sc waliendelea kutumia mipira mirefu, kusaka goli la kusawazisha, huku Al-ahly wakipoza mchezo huo.
Yanga walisawazisha goli hilo katika dakika ya 19 baada ya mlinzi wa Al-ahly, Ahmed Sayed kujifunga katika harakati ya kuokoa krosi ya Boubacry na kupeleka dakika 45 za mwanzo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Katika kipindi cha pili Al-ahly walianza kwa kutawala mpira na katika dakika ya 48 amanusura waandike goli la pili kufuatia shuti la mshambuliaji wa Al-ahly kugonga mwamba.
Kocha wa yanga Pluijim alimpumzisha Deusi Kaseke na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashuiya, huku akimtoa Amisi Tambwe na kuingia Saimon Msuva kitendo kilichopelekea Yanga kurejesha utawala wake wa mchezo.
Katika dakika ya 78 kipa wa yanga Ally Mustapha Bathezi aliumia na nkukimbizwa hospitali, na nafsi yake kuchukuliwa na Deogratius Munish 'Dida' na mpaka dakika 90 zinakamilika Yanga SC 1-1 Al-ahly.
Kwa matokeo, Yanga italazimika kwenda kushinda ugenini ili kutimiza ndoto za kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya pili katika historia yao baada ya mwaka 1998.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni