STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 9 Mei 2016

MCHEZAJI MWINGINE TENA WA CAMEROON AFARIKI UWANJANI

KIPA wa kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya Cameroon, Jeanine Christelle Djomnang amefariki dunia baada ya kuanguka wakati akifanya mazoezi ya kupasha misuli. 
 
Shirikisho la Soka la nchini hiyo-Fecafoot, limedai kuwa Djomnang mwenye umri wa miaka 26, aliugua kabla ya mchezo wa timu yake ya Femina Stars Ebolowa huko kusini mwa Cameroon jana na alifariki wakati akikimbizwa hospitali. 
 
Taarifa za awali kutoka Fecafoot zinadai kuwa mchezaji huyo alifariki kwa shambulio la moyo lakini kwasasa bado wanasubiri taarifa ya kitabibu. 
 
Taarifa hizo zinakuja siku chache baada ya mchezaji mwingine wa nchi hiyo Patrick Ekeng kufariki dunia baada ya kuanguka katika mchezo wa Ligi Kuu huko Romania. 
 
Inadaiw kuwa Djomnang alikuwa akilalamika maumivu ya kifua wakati wakijiandaa na mchezo huo wa ligi kabla ya kuanguka na kukimbizwa hospitali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox