SIKU moja baada ya kocha
George Lwandamina raia wa Zambia kutua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba wa
kuifundisha Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm ameandika barua ya
kujiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo.
Habari za kubadilishwa kwa benchi la ufundi la Yanga zilikuwepo kwa zaidi ya wiki sasa na Pluijm hakupewa taarifa yoyote hata pale alipowasili Mzambia huyo hapo jana bado uongozi wa Yanga ulisisitiza kuwa ni mwajiriwa wao halali.

Habari zinasema kwamba Pluijm
hajafurahishwa na maamuzi ya viongozi wa Yanga kumleta mbadala wake pasipo
kumpa taarifa zozote huku yeye wakiendelea kumwambia kuwa bado ni kocha wao.
Pluijm amepanga kuwaaga wachezaji wake kesho kwenye mazoezi ya asbuhi na kueleza kuwa Yanga italazimika kumlipa kocha huyo mshahara wa mwezi mmoja huku tayari zikiwepo taarifa za kwamba Lwandamina angesaini mkataba wa miaka miwili muda wowote kuanzia leo.
Maamuzi hayo yatakuwa magumu kwa timu ya Yanga ambayo keshokutwa inakabiliwa na mechi dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa Uwanja wa Uhuru ikiwa imetoka kuifunga Kagera Sugar bao 6-2 na kukusanya pointi 21 ilishika nafasi ya pili.

Pia kuna taarifa kuwa Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi atakiongoza kikosi
cha Yanga katika mechi zilizobaki hadi hapo kocha mkuu mpya atakapoanza kazi.
Taarifa za ndani kutoka Yanga
zinasema George Lwandamina raia wa Zambia ataanza kazi rasmi Novemba Mosi.
Tayari Lwandamina yuko jijini Dar es
Salaam na Kocha Hans van der Pluijm ameachia ngazi rasmi kuinoa Yang.
“Mwambusi ndiye ataendelea na
kikosi, mambo mengine yakikamilika Lwandamina ataanza kazi,” alisema.
Awali ilielezwa kwamba Pluijm
atakuwa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga kabla ya mwenyewe kuamua kujiuzulu
Zipo taarifa zinasema pia
Uongozi wa Yanga unamuondoa Pluijm na Wasaidizi wake
wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote
wazalendo na kumpa nafasi Mzambia, George Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu,
akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa
na Meneja, Sekilojo Chambua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni