KITAIFA;
MABADILIKO ya benchi la Ufundi la Yanga SC yameiva kufuatia kuwasili kwa kocha Mzambia, George Lwandamina jana tayari kusaini Mkataba.
Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi na Wasaidizi wake, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo wataondoka.
Na Mzambia, George Lwandamina atakuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.
Kocha Mzambia, George Lwandamina anatakiwa kuchukua nafasi ya Pluij Yanga
Pluijm amejikuta katika wakati mgumu baada ya Yanga kuambulia pointi 21 kati ya 30 za mechi 10 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga SC imetoa sare tatu, imefungwa mechi moja na kushinda sita tangu kuanza kwa Ligi Kuu – hiyo ikiwa ni mbali na kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Azam kwa penalti 4-1 baada ya sare ya 2-2.
Na baada ya mchezo wa Oktoba 1, wakilazimishwa sare ya 1-1 na mahasimu, Simba SC waliokuwa pungufu kwa sehemu kubwa kufuatia Nahodha wao, Jonas Mkude kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29, baadhi ya viongozi wa Yanga wamependekeza mwalimu huyo aondolewe.
Lakini habari zinasema Pluijm atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi katika mabadiliko haya.
STORI YA PILI;
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu ameamua kuachana na klabu yake ya JK Kongo, TP Mazembe baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitano.
Taarifa rasmi ya tovuti ya TP Mazembe imesema mshambuliaji huyo ameamua kufuatilia ofa mbalimbali za klabu kutoka barani Ulaya.
TP Mazembe ilifanya juhudi za kutaka kumpa mkataba mpya lakini alikataa kufanya nayo mazungumzo akisisitiza anaona ni muda muafaka wa kufuata nyayo za Mbwana Samatta barani Ulaya,
Kocha wake, Herbet Velud amemuelezea Ulimwengu kama mchezaji muhimu na licha ya kuhuzunika kwa kuondoka kwake hawezi kumlaumu kwani anaelewa kiu na ndoto zake za kusonga mbele.
” Daima Thomas Ulimwengu amecheza kwa kiwango kizuri, Namtakia mafanikio zaidi huko mbeleni. ”
Kabla ya kuondoka Lubumbashi, Ulimwengu aliitumia klabu yake ujumbe wa kuwaaga kwa kuandika.
” Katika miaka mitano, TP Mazembe imeniwezesha kukua na ninataka kuwashukuru wote walioniunga mkono na kunisaidia kushinda mataji, hawa wanaoongozwa na Rais Katumbi na Bi.
Carine, viongozi, makocha na mashabiki. Naamini TP Mazemmbe itabeba taji la Kombe la Shirikisho. Asanteni sana.
KIMATAIFA;
BEST TWEETS BAADA YA MAN UNITED KUPIGWA 4-0 NA CHELSEA JANA;
TWEETS- JINSI MOURINHO ALIVYOSAGWA MITANDAONI BAADA YA KIPIGO CHA JANA;
UNAJUA MANENO AMBAYO MOURINHO ALIMNONG'ONEZA CONTE BAADA YA MCHEZO WA JANA!!!
Meneja
wa Manchester United Jose Mourinho ameonyesha kukerwa na namna meneja
wa Chelsea Antonio Conte alivyoshangilia kwa kukera baada ya Chelsea
kuiadhibu United mabao 4-0 jana.
Magoli
kutoka kwa Pedro, Gary Cahill, Eden Hazard na N'Golo Kante yalileta
maafa kwa Mourinho aliporejea kwa mara ya kwanza kabisa Stamford Brigde
tangu alipotimuliwa mwaka jana.
Lakini
licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, mashabiki wa United ndio
walionekana kuwa na sauti zaidi hali iliyomsababisha Conte kuwaamsha
mashabiki wake kuishangilia timu yao.
Kufuatia tukio hilo, baada ya mchezo Mourinho alimfuata Conte na kumkosoa kwa kitendo chake hicho.
"Usishangilie
kwa namna hiyo ukiwa umeshinda 4-0, ingekuwa 1-0 sawa,lakini 4-0
inaumiza sana," Mourinho alimwambia Conte maneno ambayo yalinaswa na
vipaza sauti vilivyokuwa karibu.
Wakati alipoulizwa alimwambia nini Conte baada ya mchezo, Mourinho alikaa kujibu.
Kwa upande wake Conte alipoulizwa alitabasamu na kujibu: "Nadhani tuache mazungumzo binafasi yabaki kuwa binafsi, au sio."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni