
Tayari yalishaanza maneno kwa kocha wa Ufaransa Didier Deschamps kwamba ampige chini kiungo wa Manchester United Paul Pogba kwenye kikosi cha Ufaransa kilichocheza dhidi ya Uholanzi.
Nyota huyo mwenye miaka 23 amelipa fadhila za kuaminiwa na kocha wake baada ya kufunga goli pekee kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 dhidi ya Uholanzi
Akiwa umbali wa zaidi ya mita 30 kutoka golini, Paul Pogba aliachia shuti kali ambalo lilimshinda golikipa wa Everton Maarten Stekelenburg licha ya kujaribu kupangua shuti hilo.
Golikipa huyo mdachi alipambana kadri alivyoweza ili kuzuia shuti la Pogba lakini hakuweza kufanya kile ambacho alitarajia kukifanya na hatimaye kuzishuhudia nyavu zake zikicheza.
Sasa huenda mashabiki wa Manchester United wakawa na matumaini mapya ya kumuona Pagba akifunga magoli mengine kama hayo akiwa kwenye klabu yake ya Old Trafford.
STORI YA PILI;

Striker wa Crystal Palace Christian Benteke ameweka historia usiku wa October 10 kwa kufunga goli sekunde ya 7 baada mchezo kuanza wakati Ubelgiji ikicheza dhidi ya Gibraltar.
Romelu Lukaku alikosekana kwenye mchezo huo kutokana na majeraha, na kutoa nafasi kwa Benteke ambaye ameweka rekodi yake kwa kuwa mchezaji aliyefunga goli la mapema zaidi kwenye historia ya hatua za kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Davide Gualtieri wa San Marino alikuwa anashikilia rekodi hiyo baada ya kufunga goli sekunde ya 8.3 dhidi ya England November 1993.
Christian Benteke aliyeshindwa kutamba kwenye kikosi cha Liverpool liinasa pasi ya mchezaji wa Gibraltar kisha kabla ya kufunga bao kwa mguu wa kushoto.
Aliongeza bao jingine dakika mbili kabla ya mapumziko na kuifanya Ubelgiji kuwa mbele kwa magoli 3-0 hadi wakati wa mapumziko.
Benteke alikamilisha hat trick yake 55 kipindi cha pili katika mchezo huo ambao Ubelgiji ilishinda kwa magoli 6-0.
Wafungaji wengine wa magoli ya Ubelgiji ni Witsel (19’), Mertens (51’) na Hazard (79).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni