Wiki
hii historia mpya imewekwa nchini Italy baada ya mshambuliaji wa
Vicenza inayoshiriki Ligi ya Serie B, Cristian Galano kuzawadiwa kadi ya
kijana kwa kucheza mchezo wa kiungwana (fair play).
Maafisa
wa soka nchini Italy mwanzoni mwa msimu huu walitangaza matumizi ya
kadi hiyo na kusema mchezaji atayekuwa na kadi nyingi zaidi za kijana
atapewa zawadi mwishoni mwa msimu.
Kadi
hiyo ilitolewa baada ya Galano kukiri kwa mwamuzi kuwa, hakukuwa na
beki yeyote wa Virtus Entella aliyegusa mpira ambao mwamuzi Marco
Mainardi aliamuru kupigwa kona.
Rais
wa Serie B Andrea Abodi amekiri kwamba kadi hiyo ipo kama alama tu,
lakini yenye mantiki ya kuifanya ligi hiyo kuwa na mtazamo chanya
kufuatia kukabiliwa na tuhuma mbalimbali za upangaji matokeo.
"Ni
kadi ambayo ipo kama alama tu," amesema "Ni kitu rahisi tu. jambo
muhimu hapa ni kujua tu kwamba mtu hupewapindi anapofanya jambo la
kiweledi zaidi.
“Sisi
tunaamini kwamba mchezo wa soka unahitaji ujumbe weye kuijenga jamii
yenye mtazamo chanya,” Ofisa Habari wa Serie B aliongeza.
“Kumbuka mchezo huu wakati mwingine unaweza kusababisha hasira kwa watu mpaka wakatoka uwanjani.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni