Jerome Dufourg |
Baada
ya taarifa za ujio wa kocha mpya Mzambia George Lwandamina na kujiuzulu
kwa aliyekuwa koca wa timu Hans Van der Pluijm, Yanga imeendelea
kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi na kumleta Mtendaji Mkuu mpya
Jerome Dufourg kutoka nchini Ufaransa, ambaye amasaini mkataba wa miaka
mitatu.
Dufourg
ambaye vile vile amewahi kufanya kazi katika Shirikisho la Soka Rwanda
(FERWAFA) na klabu ya FC Talanta inashiriki Ligi Daraja la pili nchini
Kenya anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam wakati wowote kuanzia
leo kuanza kazi rasmi..
Mfaransa
huyo mwenye umri wa miaka 30 anatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam
mwezi ujao na kuanza kazi rasmi Novemba 19 punde tu baada ya kumalizana
na boasi wake, Yussuf Manji.
Dufourg
anasifika kwa utendaji ulio bora katika sehemu zote alizopita na jukumu
lake kubwa litakuwa ni kuhakikisha timu inakuwa na uwezo wa kujiendesha
yenye kwa maana ya mapato ya klabu yazidi matumizi.
STORI YA PILI;
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemwomba msaada Mfalme Mohammed VI wa Morocco kufadhili ujenzi wa Uwanja wa michezo mjini Dodoma utakaogharimu kiasi cha dola 80 milioni.
Ombi hilo ameliwasilisha
leo wakati wa halfa ya kumkaribisha Mfalme huyo aliyekuja nchini kwa
ziara ya kibiashara na tayari amekubali ombi la Rais Magufuli.
Ujenzi huo utaifanya Tanzania kuwa na viwanja viwili vya kisasa, Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam unaoingiza watu 60,000 uliojengwa wakati wa uongozi wa Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa na huo utakaojengwa Dodoma ambako serikali kuu inahamia.
Serika ya Magufuli inapaswa kuhamia mjini Dodoma kuanzia Novemba Mosi ambapo sasa miundombinu ya kisasa itapaswa ijengwe huko na si Dar es Salaam ambayo itabaki na ofisi za kawaida.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni