Kipa wa Mbao Emmanuel
Mseja aliokoa michomo kadhaa iliyokuwa ikielekea wavuni ambapo dakika ya 14
alipangua shuti la Laudit Mavugo kabla ya kuokoa michomo mingine dakika za 24
na 32
Kuingia kwa mshambuliaji
Fredrick Blagnon kuliongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Simba lakini
bado walinzi wa Mbao walikuwa makini kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi kwa
namna yoyote.
Kiungo Muzamiru Yassin aliifungia Simba bao la ushindi dakika ya 86 baada ya kupokea pasi safi ya kichwa toka kwa Blagnon na kuingia ndani ya eneo la hatari akiwa peke yake bila upinzani wowote kutoka kwa Wachezaji wa Mbao na kuuweka mpira nyavuni.
Simba iliwatoa Mavugo na Ibrahim Ajib nafasi zao zikachukuliwa na Blagnon pamoja na Mohamed Ibrahim huku Mbao ikiwatoa mkongwe Hussein Swedi na Pius Buswita na kuwaingiza Boniface Maganga na Frenk Damas.

Kikosi cha Simba: Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohamed Hussein, Murshid Juuko, Jonas Mkude, Method Mwanjale, Shiza Ramadhani, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib, Mwinyi Kazimoto.
Mbao: Emmanuel Mseja, Steve Mganya, Steve Kigoha, Asante Kwasi, Pius Buswita, Youssouf Ndikumana, Robert Magadula, Salmin Hoza, Emmanuel Mvuyekure, Hussein Swedy, Dickson Ambundo

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni