
Baada
ya Uganda kupangwa Kundi D sambamba na timu za Misri, Ghana, pamoja na
Mali kwenye micuano ya AFCON 2017, kocha wa Uganda Cranes Micho
Sredojević ametoa wito kwa serikali kuhakikisha timu inapata support ya
kutosha kwa ajili ya maandalizi ya mapema.
Licha ya timu yake kupangwa kwenye Kundi gumu, Micho hana budi bali ni kupambana na changamoto iliopo mbele yake.
“Hakuna
namna ya kukwepa, unaweza ukasema pengine ndiyo mwisho wetu, ni sawa na
Kundi tulilopo kwenye Kombe la Dunia lakini safari hii ni fainali za
AFCON dhidi ya Ghana na Misri. Ni kundi gumu lenye ushindani,” alisema
Micho mara baada ya draw ya upangaji makundi kukamilika.
Ghana
walipoteza kwenye mchezo wa fainali katika michuano iliyopita ya FCON
iliyofanyika Equatorial Guinea 2015 dhidi ya Ivory Coast. Misri ni nchi
yenye uchu ikiwa imeyakosa mashindano hayo kwa miaka misimu mitatu
iliyopita, lakini wakiwa ni mabingwa mara tatu mfululizo waliopta, Mali
ndani ya fainali tatu za AFCON wameshika nafasi ya tatu mara mbili, ni
kundi gumu.
Ghana
na Uganda zilitoka suluhu kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kundi E kuwania
kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 na wanatarajia
kucheza mara mbili dhidi ya Misri baada ya michuano ya AFCON kumalizika.
“Ukiangalia
kila kitu, utaona tunatakiwa kuanza maandalizi sasa kwa upendo na
support kutoka waganda wote, wachezaji na wote wenye wajibu wa kuiandaa
timu yetu kuwa timu yenye ushindani, hapa nafikiria maandalizi pamoja na
mechi za kirafiki ambapo tutakuwa makini na kila taarifa. Naamini
katika soka hakuna kinachoshindikana bali kila kitu kinawezekana.”
“Ninaiamini
timu na wachezaji tulionao, naamini katika kile tunachokifanya,
ninaamini serikali ya Uganda itatusaidia kuhakikisha tunaliwakisha taifa
katika njia bora.”
“Hatua
tuliyofikia ni nusu ya safari, ili safari yetu ikamilike tunahitaji
kuanza maandalizi sasa, tunastahili kuwa hapa lakini tunahitaji kuonesha
hilo kwa vitendo tukiwa uwanjani na si kwa kuongea.”
Uganda
wataanza kampeni yao kwa mchezo wao wa ufunguzi January 17 dhidi ya The
Black Stars, kisha watashuka tena uwanjani kukabiliana na mapharao wa
Msri January 21 kabla ya kuhitimisha hatua ya makundi dhidi ya Mali
January 25.
Makundi;
MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA UEFA JANA HAYA HAPA
REKODI YA MESSI;

Lionel Messi amefunga hat-trick wakati Barcelona ikiaangamiza
Manchester City kwenye mchezo wa Champions League wakati Pep Guardiola
akirejea kwenye klabu yake ya zamani.
City walipambana kipindi cha kwanza lakini walifanya makosa mengi ya
wazi dhidi ya kikosi cha Barcelona ambacho ndani yake kilikuwa na Messi
aliye rejea kutoka majeruhi.
Fernandinho alianguka ndani ya box na kumpa nafasi Messi kupachika
bao la pili kabla ya Kelvin de Bruyne kupoteza mpira na kumruhusu
Iniesta kumtengenezea muargentina huyo kufunga bao la pili.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa wageni ambapo golikipa wao Claudio Bravo
alizawadiwa kadi nyekundu kwa kudaka mpira akiwa nje ya box kisha
dakika moja baadaye Messi akapachika bao jingine.

Barcelona pia walibaki 10 uwanjani kwa dakika 15 za mwisho baada ya
Jeremy Mathieu ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Gerrard Pique
kuoneshwa kadi ya pili ya njano kwa kumfanyia madhambi Raheem Sterling.
Willy Caballero aliokoa mchomo wa Neymar lakini nyota huyo wa Brazil
akafunga goli dakika moja baadaye kukamilisha ushindi wa magoli 4-0 wa
miamba hiyo ya La Liga.
Ushindi huo uaifanya Barcelona kuendeleza ushindi kwa 100% katika
Kundi C na kuendelea kuongoza kwa tofauti ya pointi tano na Manchester
City.
Hiki kilikuwa ni kipigo kingine kwa Guardiola akirejea Nou Camp.
Akiwa kocha wa Barcelona, aliisaidia timu hiyo kutwaa jumla ya mataji 14
lakini sasa amepoteza mara mbili dhidi ya klabu hiyo ya Hispania.
Alichezea kichapo cha magoli 3-0 kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali
ya UEFA Champions Legue akiwa kocha wa Bayern Munich.
- Lionel Messi amefunga magoli 15 katika mechi 13 za Champions League dhidi ya timu za England.
- Manchester City wamechezea kipigo kikubwa zaidi kwenye michuano ya Champions League, kwa mara ya kwanza wamefungwa magoli manne.
- Goli la kwanza la kwenye mchezo huo lilikuwa ni goli la 100 kwa safu ya MSN kwenye mashindano yote kwa mwaka 2016.
- Messi kwa sasa anaongoza orodha ya wafungaji katika viwanja vya nyumbani kwenye michuano ya Ulaya akiwa mefunga magoli 50.
- Pep Guardiola ameruhusu magoli 9 kwenye mechi tatu za Champions League dhidi ya Barcelona tangu alivyoondoka kwa miamba hiyo ya Catalan.
- Barcelona wamekosa mikwaju 11 ya penati kati ya 27 ambayo wamepata katika michuano yote tangu kuanza kwa msimu wa 2015-16.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni