MSHAMBULIAJI wa Obrey
Chirwa ameanza kuwajibu waliokuwa wakimbeza kuwa ni 'galasa' baada ya leo
kufunga tena kwenye ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Toto African mchezo
uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Chirwa alikuwa katika wakati mgumu baada ya kuchelewa kufunga tangu
aliposajiliwa toka FC Platinum ya Zimbabwe kwa dau la sh 200 milioni huku wengi
wakisema mshambuliaji huyo hakustahili kununuliwa kwa pesa hiyo kulinganisha na
ufanisi wake uwanjani. Chirwa alifunga goli lake la kwanza kwenye ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mzimbabwe huyo aliipatia ya Yanga bao la kwanza dakika ya 29 kwa kichwa cha mkizi akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Simon Msuva pembeni kidogo ya eneo la hatari.
Msuva aliifungia Yanga bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 55 baada ya Deus Kaseke kuangushwa na beki wa Toto kwenye eneo la hatari.
Yanga imepanda hadi nafasi ya tatu baada ya kufikisha alama 18 katika michezo tisa iliyoshuka dimbani pointi tano nyuma ya vinara Simba wanaongoza.
Matokeo mengine ya mechi za Leo
African Lyon 0-2 Majimaji
Ruvu Shooting 1-1 Mwadui FC
Ndanda FC 1-1 Mbeya City
Tanzania Prisons 2-1 Stand United.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni