TIMU ya Yanga imepangiwa kucheza na MC Alger kutoka Algeria katika hatua ya 32 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika kwa mujibu wa ratiba iliyotoka muda mfupi uliopita.
Mchezo wa kwanza utafanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam kati ya Aprili 7 na 9 kabla ya mechi ya marudiano itayofanyika nchini Algeria kati ya Aprili 14 na 16.
MC Alger iliwahi kuchukua ubingwa wa ligi ya mabingwa Afrika mwaka 1976 ambapo kwenye msimamo wa ligi msimu huu inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 35 baada ya kushuka dimbani mara 20.
Yanga inatakiwa kutoka na ushindi katika mchezo huo ili kufuta uteja kwani mara kadhaa timu zinazotoka kwenye nchi za Kiarabu zimekuwa zikisumbua sana klabu za Tanzania.
Yanga ilitolewa na Zanaco FC ya Zambia kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika kwa faida ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya bao moja nyumbani kabla ya kulazimishwa sare ya bila kufungana mjini Lusaka Jumamosi iliyopita na kutupwa kwenye michuano hiyo.
Ratiba kamili ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika
Yanga SC vs MC Alger
TP Mazembe vs JS Kabyle
FC Leopards vs Mbabane Swallows
C.F Mounana vs ASES Mimosas
F.U.S vs M.A.S
Rangers vs Zesco United
Rail Club K vs CS Sfaxien
Bidvest Wits vs Smouha
CNaps vs C.R.D Libolo
KCCA vs El Masry
Gambia Ports vs Al Hilal Obeid
ASPL 2000 vs Club Africain
River United vs Rayon Sports
BYC vs Supersport United
AS Tanda vs Platinum Stars
Horoya vs IR Tanger.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni