Wenyeji Mbao walipata bao la kuongoza kupitia kwa George Sanguja dakia ya 20 aliyefunga kwa shuti kali kutokea upande wa kulia.
Bernard Evaristu akaipeleka mbele zaidi Mbao kwa bao la pili kabla
ya kipindi cha kukatika pale alipowazidi maarifa walinzi wa Simba
waliojichanganya na kumruhusu kuzitikisa nyavu za Manyika.
Blagnon aliyerejea hivi karibuni akitokea Oman alifunga mabao hayo dakika ya 82 na 91 na kisha Yassin Mzamiru akafunga bao la ushindi katika dakika ya mwisho ya muda wa majeruhi.
Kwa ushindi huo Simba inarudi kileleni kwa kuipindua Yanga kwa tofauti ya pointi mbili japo wapinzani wao wana mchezo mmoja mkononi
Katika mchezo wa leo dhidi ya Mbao, kocha huyo raia wa Cameroon amewaacha nje ya kikosi wachezaji sita huku mmoja, Abdi Banda akiachwa kwa sababu amesimamishwa kucheza na Kamati ya Masaa 72.
Katika kikosi kilichocheza dhidi ya Kagera Sugar, Daniel Agyei, Jonas Mkude, Laudit Mavugo, .Ibrahim Ajibu, na Said Ndemla walianza kikosi cha kwanza lakini leo hawapo.
Nafasi zao zimechukuliwa na Peter Manyika, Juma Liuzio, Hamad Juma, Mohamed Ibrahim, Pastory Athanas na Janvier Bokungu aliyekuwa majeruhi.
Ushindi huo unairejesha Simba kileleni, ikifikisha pointi 58 baada ya kucheza mechi 26, wakati mabingwa watetezi, Yanga wanarudi nafasi ya pili kwa pointi zao 56.
Kikosi cha Mbao FC kilikuwa; Erick Ngwengwe, Asante Kwasi, David Mwasa, Boniphace Maganga, Yussuf Ndikumana, Vincent Philipo, George Sangija, Salmin Hoza, Pius Buswita, Ibrahim Njohole na Everigeston Bernard.
Simba SC; Peter Manyika, Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Janvier Bokungu, James Kotei, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Juma Luizio, Mo Ibrahim na Pastory Athanas.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni