
Tambwe aliyekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti ataongoza safu ya ushambuliaji akisaidiana na Donald Ngoma ambaye amerejea kikosini wiki iliyopita kwenye mchezo wa hatua ya kwanza ambao Yanga ilishinda bao moja katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka kesho saa 12 jioni kwa ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai tayari kwa mchezo ambao sare au ushindi wa aina yoyote utaifanya Yanga kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Wachezaji watakaosafiri ni Makipa Deogratius Munishi na Beno Kakolanya . Mabeki ni Nadir Haroub , Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondan.
Viungo ni Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimon Msuva, Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin huku
washambuliaji wakiwa ni Tambwe na Ngoma.
Mbali na Chirwa wachezaji wengine watakaokosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali ni Justine Zulu, Malimi Busungu, Matheo Antony, Ally Mustapha, Pato Ngonyani na Yusuph Mhilu.
Yanga itashuka dimbani wikiendi ijayo nchini Algeria na endapo itafanikiwa kuwaondoa Alger basi itaingia moja kwa moja katika hatua ya makundi ya michuano hiyo kama ilivyokuwa mwaka jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni