
Wachezaji wa Serengeti walifanyiwa vipimo Aprili 25, mwaka huu katika Hospitali ya Cardiologique De Rabat ambapo Shirikisho la Soka la Tanzania lilithibitisha kufanyika kwa zoezi hilo ambalo ni moja ya masharti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambao ndiyo waandaaji wa michuano hiyo.
Serengeti Boys ambayo imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya michuano hiyo, Mei 7, mwaka huu itaelekea Gabon ambako ndipo michuano itakapofanyika ikiwa imepangwa Kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola, wakati Kundi A lina timu za wenyeji, Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni