STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 3 Mei 2017

MSIKILIZE AVEVA MWANZO MWISHO AKIZUNGUMZA ISHU YA KWENDA KULALAMIKA FIFA JUU YA WANAYOFANYIWA NA TFF



RAIS wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) haikutenda haki kumfungia msemaji wa timu hiyo Haji Manara bila kumpa nafasi ya kumsikiliza kutokana na kupata dharura.
  Aprili 23 kamati hiyo chini ya Makamu Mwenyekiti  Wakili Jerome Msemwa ilimfungia Manara mwaka mmoja na faini ya Shilingi milioni tisa kwa kosa la kutamka maneno yasiyo na staha kwa viongozi wa Shirikisho hilo.

  Aveva alisema hayo mbele ya wandishi wa habari kuwa hakukuwa na haraka kutoa hukumu hiyo bila ya kumsikiliza msemaji huyo kwakuwa klabu ilipeleka barua TFF kuomba hukumu isogezwe mbele kwani Manara alikuwa nje ya mji akishughulikia mambo yake.

  “Hili suala kama uongozi wa Simba limetushangaza sana. Hatukuona sababu ya Kamati ya nidhamu kuwa na haraka wa kiasi hicho kutoa hukumu bila kumsikiliza mshitakiwa ambaye klabu ilikuwa imemtolea udhuru.

  “Kuna mambo mengi yanachelewa kutolewa maamuzi lakini suala la Manara aliyekuwa akiitetea klabu limeamuliwa haraka bila hata kumsikiliza mshitakiwa,” alisema Aveva.

  Pia Aveva alisema wamesikia fainali ya michuano ya kombe la FA itanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ambapo kwa upande wao wamesema kwa ukubwa wa mshindano hayo yalipaswa kufanyikia Uwanja wa Taifa ila hawana kipingamizi na maamuzi ya TFF.

Lakini pia amesema wanasubiri kupewa barua na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayoonyesha kweli wamepokwa pointi tatu za mchezo dhidi ya Kagera Sugar ili wakashitaki katika Mahakama ya usuluhishi ya FIFA (CAS) .

Simba ambayo ilipoteza mchezo huo mabao 2-1, ilikabidhiwa pointi tatu baada kamati ya usimamizi na uendeshwaji wa ligi (Kamati ya saa 72) kujiridhisha kuwa Kagera walimchezesha beki Mohamed Fakih ambaye alikuwa na kadi tatu za njano kabla ya mchezo huo pointi ambazo baadae zilirejeshwa kwa Kagera na kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji.


Rais wa klabu hiyo Evans Aveva amesema hawawezi kukubali kuona timu yao inaonewa tena na TFF na kwa kuanzia wanasubiri wapewe barua ya kuporwa pointi tatu hizo ili wapeleke malalamiko yao CAS.


“Tumeonewa mara nyingi, mfano suala la wachezaji Mbaraka Yusuph, Hassan Kessy na Ramadhan Singano ‘Messi’ walikuwa wachezaji wetu halali lakini TFF wakawaidhinisha kucheza timu nyingine, huu ni uonevu tumechoka kuonewa tunaenda FIFA,” alisema Aveva.


Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 59 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 56 na michezo miwili mkononi ambayo ikishinda yote itaizidi Simba kwa pointi tatu.

Maoni 1 :

  1. Thanks for sharing. If you want to watch the World Cup live matches for free, I just read a post and hope that helps too: Top 10 VIPBox Alternatives to Watch Live Sports

    JibuFuta

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox