Timu ya Soka ya Everton Inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza wamethibitisha kuwa watatua nchini mwezi wa saba kwa Ajili ya mchezo wa Kirafiki utakaochezwa tarehe 17.
Taarifa rasmi kutoka klabuni humo inasema kuwa Everton itautumia mchezo huo kama maandalizi yao ya kujiandaa na msimu wa Mwaka 2017-18 na vilevile ni kama kusherehekea mkataba wao na kampuni nguli ya Kamari ya SportPesa
Mtanange huo utapigwa kunako Uwanja wa taifa unaoingiza mashabiki 60000 walioketi vitini ambapo muda wa kuanza pambano bado haujawekwa bayana
Everton itakuwa klabu ya kwanza ya ligi Kuu nchini Uingereza kutua mchini (Afrika mashariki) na kukipiga katika Ardhi ya Tanzania ambapo itacheza na Bingwa Wa Kombe la SportPesa Super Cup
Taarifa Za ndani zinasema Everton watakuja na kikosi chao kamili kikiongozwa na Kocha Ronald Koeman
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni