BEKI
wa Simba SC, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amefanikiwa kushinda tuzo ya
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika sherehe
zilizofanyika usiku wa Jumatano ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Tshabalala
anayecheza upande wa kushoto, baada ya msimu mzuri akiiwezesha Simba
kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu nyuma ya mahasimu, Yanga
walioibuka mabingwa, amewabwaga
Aishi Manula wa Azam, Simon Msuva wa Yanga, Shiza Kichuya wa Simba na Haruna Niyonzima wa Yanga.
Lakini
kiungo wa Rwanda, Niyonzima ‘akainua kwapa’ kwa kunyanyua tuzo ya
Mchezaji Bora wa Kigeni, akiwashinda beki Mzimbabwe wa Simba, Method
Mwanjali na kiungo Mrundi wa Mbao FC, Yusuph Ndikumana.
Manula
naye akainua tuzo ya Kipa Bora akiwashinda Owen Chaina wa Mbeya City na
Juma Kaseja wa Kagera Sugar, wakati Msuva amebeba tuzo ya Mfungaji Bora
kwa pamoja na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting baada ya wote
kufungana kwa mabao 14 kila mmoja.
Kocha kijana, Mecky Mexime amewashinda makocha wa kigeni, Mcameroon wa Simba, Joseph Omog na Ettiene Ndayiragije wa Mbao FC.
Mshambuliaji
chipukizi wa Kagera Sugar, Mbaraka Yussuf Abeid ameshinda tuzo ya
Mchezaji Bora Chipukizi wa Ligi Kuu akiwaangusha Shaaban Iddi wa Azam FC
na Mohammed Issa ‘Banka’ wa Mtibwa Sugar.
Shaaban Iddi naye akawaangusha mchezaji mwenzake wa Azam, Abdallah Masoud ‘Cabaye’ na Mosses
Kitambi wa Simba katika tuzo ya Mchezaji Bora wa U-20, inayojulikana
kama tuzo ya Ismail Khalfan wakati Shiza Kichuya akashinda tuzo ya Bao
Bora la Msimu alilofunga kwenye mechi dhidi ya Yanga katika ushindi wa
2-1 akiyazidi mabao ya Peter Mwalyanzi wa African Lyon na Zahoro Pazi wa
Mbeya.
Refa Bora ni Elly Sasii wa Dar es Salaam aliyewashinda Shomari Lawi wa Kigoma na Hance
Mabena wa Tanga, wakati Tuzo ya Heshima imekwenda kwa gwiji Kitwana
Manara aliyeanza kucheza kama kipa na baadaye mshambuliaji kwa mafanikio
makubwa timu ya taifa na klabu ya Yanga na Mwadui FC imeshinda tuzo ya
timu yenye Nidhamu.
Kikosi
Bora cha Wachezaji wa Ligi Kuu wa msimu ni; Aishi Manula (Azam), Salum
Kimenya (Prisons), Mohammed Hussein (Simba), Yakoub Mohammed (Azam FC),
Method Mwanjali (Simba), Kenny Ally (Mbeya City), Simon Msuva (Yanga),
Haruna Niyonzima (Yanga), Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), Abdulrahman
Mussa (Ruvu Shooting) na Shiza Kichuya (Simba).
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatano, 24 Mei 2017
Home
/
Unlabelled
/
WASHINDI WOTE WALIO JINYAKULIA TUZO JANA KWENYE MSIMU WA VPL WAPO HAPA, KICHUYA, NIYONZIMA KIDEDEA
WASHINDI WOTE WALIO JINYAKULIA TUZO JANA KWENYE MSIMU WA VPL WAPO HAPA, KICHUYA, NIYONZIMA KIDEDEA
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni