STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 17 Aprili 2015

CHELSEA KINARA WA EPL LAKINI PIA WANAONGOZA KWA UTOVU WA NIDHAMU ENGLAND


Takwimu zilizotolewa na maafisa wa mchezo wa kiungwana wa FA zinaeleza kuwa Chelsea ni timu inayoongoza kutoheshimu maamuzi ya waamuzi katika ligi kuu England, huku makocha wa timu hiyo wakishika nafasi ya pili kwa utovu wa nidhamu wakati wa mechi.
Liverpool imetajwa kuwa klabu yenye heshimu kubwa kwa waamuzi  katika kipengele hicho kilichobeba alama saba ikifuatiwa na Burnley na West Brom.
Klabu za Arsenal na Stoke City zipo katikati katika orodha hiyo ambapo kanuni zinaeleza kuwa kitendo cha kuheshimu maamuzi yenye utata bila kugoma au kumzonga muamuzi kinaipa timu alama saba wakati tabia ya kukubali maamuzi halafu kuonesha ishara za kutoheshimu zinatolewa alama sita.
FA wanatoa alama kwa kuangalia maeneo sita ambayo ni kadi nyekundu na njano, mchezo mzuri, heshima kwa wapinzani, heshima kwa waamuzi, tabia ya maafisa wa timu na mashabiki.
Alama kumi zinatolewa kwa kadi nyekundu ambapo timu inapunguziwa alama moja kwa kadi ya njano na alama tatu kwa kadi nyekundu.
Mchezo mzuri una alama kumi zinazotolewa kwa kucheza soka la kuvutia, kushambulia sana na kushinda, lakini timu ikitumia mbinu za kujilinda na udanganyifu alama zinapunguzwa.
Alama saba zinatolewa katika kipengele cha heshima kwa wapinzani kinachohusisha kuwaheshimu wachezaji pinzani na kuonesha mchezo wa kiungwana, wakati alama saba pia zinatolewa kwa kuheshimu waamuzi  na maafisa wa mechi.

Alama sita zinatolewa kwa maafisa wa timu wakiwemo makocha dhidi ya waamuzi, wakati alama kumi  zinatolewa kwa tabia ya mashabiki ambapo alama zote  zinatolewa kwa  mashabiki wanaokubali matokeo, wakati wakitumia  lugha ya matusi kwa wachezaji, waamuzi na kuwatishia mashabiki pinzani alama zinapounguzwa. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox