STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 17 Aprili 2015

KANE, HAZARD KUGOMBEA TUZO MBILI UINGEREZA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Harry Kane ni mmoja kati ya wachezaji wanne walioteuliwa katika orodha zote mbili za kugombea tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa wa mwaka na tuzo ya mchezaji bora anayechipukia. Golikipa wa Manchester United David De Gea, mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard na kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho nao pia wanaweza kushinda tuzo hizo mbili. Mshambuliaji wa Arsenal Alexis sanchez na Diego Costa wa Chelsea ndio wanakamilisha orodha ya tuzo ya wakubwa. Hii ni mara ya kwanza wachezaji wanne kuteuliwa kugombea tuzo zote mbili. Hazard anaingia katika orodha hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo akiwa tayari ameshapoteza kwa Gareth Bale na Luis Suarez.
Mchezaji bora wa kiume:
Diego Costa (Chelsea)
David De Gea (Manchester United)
Philippe Coutinho (Liverpool)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Alexis Sanchez (Arsenal)
Mchezaji Bora wa kiume chipukizi:
Thibaut Courtois (Chelsea)
Philippe Coutinho (Liverpool)
David De Gea (Manchester United)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Raheem Sterling (Liverpool)
Mchezaji bora wa mwaka -wanawake:
Eniola Aluko (Chelsea)
Lucy Bronze (Manchester City)
Jess Clarke (Notts County)
Karen Carney (Birmingham City)
Kelly Smith (Arsenal)
Ji So-yun (Chelsea)
Mchezaji bora chipukizi -wanawake:
Freda Ayisi (Birmingham City)
Hannah Blundell (Chelsea)
Aoife Mannion (Birmingham City)
Nikita Parris (Manchester City)
Leah Williamson (Arsenal)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox